01. Hadiyth “Laiti watu wangelijua yanayopatikana katika adhaana… “

231 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´an) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لو يعلم الناسُ ما في النداءِ والصفِّ الأولِ، ثم لم يجدوا إلا أنْ يَسْتَهِموا عليه؛ لاسْتهموا، ولو يعلمون ما في التَّهجيرِ؛ لاسْتَبَقوا إليه، ولو يعلمون ما في العَتَمةِ والصبحِ؛ لأتوهما ولو حَبْواً

“Laiti watu wangelijua yanayopatikana katika adhaana na ile safu ya kwanza kisha wasipate namna ya kuyaendea isipokuwa kwa kuyapigia kura, basi wangeyapigia kura. Na laiti wangelijua yanayopatikana katika kuiendea swalah mapema, basi wangeliiharakia. Laiti wangelijua yanayopatikana katika swalah ya usiku na Subh, basi wangeziendea ijapo kwa kutambaa.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/212)
  • Imechapishwa: 21/02/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy