Kuoga kumeshatajwa katika mlango wa kabla yake kupitia Hadiyth ya Salmaan al-Faarisiy, Aws bin Aws na ´Abdullaah bin ´Amr.

704- ´Abdullaah bin Abiy Qataadah amesema:

“Baba yangu aliingia wakati nilipokuwa nikioga kwa ajili ya ijumaa. Akasema: “Unaoga kwa sababu ya janaba au kwa sababu ya ijumaa?” Nikasema: “Ni kwa ajili ya janaba.” Ndipo akasema: “Basi oga mara nyingine. Kwani hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Atakayeoga siku ya ijumaa basi atakuwa katika hali ya twahara mpaka ijumaa nyingine.”  [1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw”. Mlolongo wa wapokezi wake unakaribia kuwa mzuri. Ibn Khuzaymah ameipokea katika “as-Swa”iyh” yake na akasema:

“Hadiyth hii ni geni. Hakuna mwengine mbali na Haaruun (Ibn Muslim) aliyeipokea.”

Ameipokea vilevile al-Haakim kwa tamko la at-Twabaraaniy na akasema:

“Ni Swahiyh kwa mujibu wa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.”

Ameipokea Ibn Hibaan kwa tamko lisemalo:

“Atakayeoga siku ya ijumaa basi hatoacha kuwa na twahara mpaka ijumaa nyingine.”

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/441)
  • Imechapishwa: 17/01/2018