07 – Abu Ayyuub al-Aswaariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kusema:
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌم
“Hapana mwabudiwa isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana na mshirika. Ufalme Wake na himdi Zake na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.”
mara kumi, anakuwa ni kama ambaye ameacha watumwa wanne kutoka katika kizazi cha Ismaa´iyl.”[1]
Kuna maafikiano juu yake.
8 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

mara mia kwa siku, basi analingana na aliyeacha watumwa kumi, ataandikiwa thawabu mia moja, atafutiwa makosa mia moja, atakingwa na shaytwaan katika siku hiyo mpaka ifike jioni na wala hakuna mtu ambaye atakuja na kitu bora zaidi kuliko alichofanya isipokuwa mtu ambaye amefanya zaidi kuliko yeye.”[2]
Kuna maafikiano juu yake.
MAELEZO
Hadiyth hii inafahamisha fadhilah za dhikr hii:

na kwamba mwenye kuisema mara kumi ni kama ambaye ameacha nafsi nne katika kizazi cha Ismaa´iyl. Maana yake ni kwamba ni kama ambaye ameacha huru watumwa kwa ajili ya Allaah (Ta´ala). Ni jambo linalotambulika kuwa kule kuwaacha kwake huru kunamlinda na Moto. Kuacha mtumwa huru kumefanywa ni kifutio cha dhambi kwa mwenye kuua nafsi. Na mwenye kusema hivo mara mia kwa siku basi anapata faida tano:
1 – Analingana na aliyeacha huru watumwa mia.
2 – Anapata thawabu mia.
3 – Anafutiwa makosa mia.
4 – Siku hiyo analindwa kutokana na shaytwaan.
5 – Hakuna yeyote atakuja na kitu bora zaidi kuliko alichofanya isipokuwa mtu ambaye amefanya zaidi kuliko yeye. Hadiyth inafahamisha pia kwamba akizidisha idadi hiyo basi anapata thawabu ya ziada hiyo. Ni mamoja zaidi hiyo inatokana na dhikr au matendo mema.
[1] al-Bukhaariy (6404) na Muslim (2693).
[2] al-Bukhaariy (6403) na Muslim (2691).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 15-16
- Imechapishwa: 28/09/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 15-16
Imechapishwa: 28/09/2025
https://firqatunnajia.com/01-fadhilah-za-laa-ilaaha-illa-allaah/