06. Allaah anajifakhari juu ya wenye kumtaja mbele ya Malaika

6 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mu´aawiyah alijitokeza kwa duara msikitini akasema: “Ni kipi kimekukazeni?” Wakasema: “Tumekaa kwa ajili ya kumtaja Allaah.” Akasema: “Apeni kwa Allaah hakuna kingine kilichokukazeni isipokuwa hicho?” Wakasema: “Tunaapa kwa Allaah hakuna kilichotukaza isipokuwa hicho.” Akasema: “Mimi sijakutakeni muape kwa kukutuhumuni, lakini hakuna yeyote ambaye anayo hadhi kama nilionayo mimi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) japo udogo wangu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatokezea duara moja ya Maswahabah akasema: “Ni kipi kimekukazeni?” Wakasema: “Tumekaa kwa ajili ya kumtaja Allaah.” Akasema: “Apeni kwa Allaah hakuna kingine kilichokukazeni isipokuwa hicho?” Wakasema: “Tunaapa kwa Allaah hakuna kilichotukaza isipokuwa hicho.” Akasema: “Mimi sijakutakeni muape kwa kukutuhumuni, lakini nimejiliwa na Jibriyl ambaye amenieleza ya kwamba Allaah anajifakhari kwa ajili yenu mbele ya Malaika.”

Ameipokea Muslim[1].

MAELEZO

Hadiyth inafahamisha fadhilah za wenye kumtaja Allaah na kwamba Allaah anajifakhari juu yao mbele ya Malaika. Kwa maana ya kwamba anawasifu na anawatajia ubora wao.

[1] Muslim (2701).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 14
  • Imechapishwa: 28/09/2025