20 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

“Allaah pekee anatutosheleza na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa.”

neno hili lilisemwa na Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alipotupwa ndani ya moto na alilisema Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoambiwa:

الَّذِينَ قالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزادَهُمْ إِيماناً وَقالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

”Wale ambao waliambiwa na watu: “Hakika watu wamekusanyika dhidi yenu hivyo basi waogopeni”; yakawazidishia imani na wakasema: “Allaah pekee anatutosheleza na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa.“[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Maneno haya ni miongoni mwa mambo yenye nguvu zaidi kukusaidia dhidi ya adui. Maana yake ni kwamba Allaah anatutosha na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa. Miongoni mwa ubora wa maneno haya ni kwamba yamesemwa na wapenzi wa Allaah wawili wa hali ya juu; Ibraahiym na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam). Kwa hivyo inapendeza mtu akithirishe kuyasema. Maneno hayo yamepokelewa miongoni mwa zile adhkaar za asubuhi na jioni kupitia katika Hadiyth ya Abu Dharr, ambayo mwalimu wetu Shaykh Ibn Baaz ameyafanya ni yenye kutoka kwake, ambaye amesema:

“Mwenye kusema mara saba kunapopambazuka na kunapoingia jioni:

حَسْبِـيَ اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُوَ عَلَـيهِ تَوَكَّـلتُ وَهُوَ رَبُّ العَرْشِ العَظـيم

”Ananitosheleza Allaah, hapana mungu wa haki mwengine isipokuwa Yeye, Kwake Yeye ni mwenye kutegemea na Yeye ni Mola wa ´Arshi tukufu.”,

basi itamtosheleza katika mambo yake yanayomtia hamu.”[2]

[1] al-Bukhaariy (4563).

[2] Abu Daawuud (5081). Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (26/25) ya Ibn Baaz.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 27
  • Imechapishwa: 01/10/2025