19 – Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:
“Tulikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema: “Hivi anashindwa mmoja wenu kila siku kuchuma mema elfu?” Akamuuliza muulizaji katika wale wale waliokuwa wameketi kwake: “Ni vipi atachuma mmoja wetu mema elfu?” Akasema: “Asabihi Tasbiyh mia ambapo aandikiwe mema elfu moja au afutiwe makosa elfu moja.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Hadiyth inafahamisha kuwa jema moja linalipwa mara kumi mfano wake. Allaah amesema ndani ya Qur-aan:
مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا
“Atakayekuja kwa tendo jema basi huyo atapata thawabu kumi mfano wake.”[2]
Akisabihi Tasbiyh mia moja, basi Allaah anamwandikia mema mia moja na jema moja linalipwa mara kumi mfano wake ambapo jumla inakuwa mema elfu moja. Hiyo ni fadhilah na wema wa Allaah (Ta´ala).
[1] Muslim (2697).
[2] 06:160
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 24-25
- Imechapishwa: 01/10/2025
19 – Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:
“Tulikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema: “Hivi anashindwa mmoja wenu kila siku kuchuma mema elfu?” Akamuuliza muulizaji katika wale wale waliokuwa wameketi kwake: “Ni vipi atachuma mmoja wetu mema elfu?” Akasema: “Asabihi Tasbiyh mia ambapo aandikiwe mema elfu moja au afutiwe makosa elfu moja.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Hadiyth inafahamisha kuwa jema moja linalipwa mara kumi mfano wake. Allaah amesema ndani ya Qur-aan:
مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا
“Atakayekuja kwa tendo jema basi huyo atapata thawabu kumi mfano wake.”[2]
Akisabihi Tasbiyh mia moja, basi Allaah anamwandikia mema mia moja na jema moja linalipwa mara kumi mfano wake ambapo jumla inakuwa mema elfu moja. Hiyo ni fadhilah na wema wa Allaah (Ta´ala).
[1] Muslim (2697).
[2] 06:160
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 24-25
Imechapishwa: 01/10/2025
https://firqatunnajia.com/12-unashindwaje-kila-siku-kujichumia-mema-elfu-moja/