01. Dibaji ya adh-Dhahabiy ya ”al-´Uluww”

Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah; maandalizi ya kukutana na Allaah. Ee Mola, wepesisha, usaidie, ukamilishe na nimalizie kwa kheri katika usalama wake. Ee Mkarimu! Himdi zote anastahiki Allaah, Aliye juu, Mtukufu, Mola wa ´Arshi tukufu, juu ya neema Zake zilizoenea, zilizo za wazi na zilizojificha. Himdi zote njema anastahiki Allaah juu ya neema ya Tawhiyd. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki mwingine isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika; shahaadah ambayo inapelekea kuzidishiwa katika fadhilah Zake. Na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake, mwisho wa Manabii na mwombezi wa siku Nzito. Ee Allaah msifu yeye na kizazi chake – swalah ambayo naihifadhi juu ya siku ya Kitisho.

Ama baada ya haya, mwaka wa 698 nilikusanya Hadiyth na mapokezi kuhusu Ujuu. Hata hivyo nikapitwa kuyazungumzia baadhi ya mambo na kwa ajili hiyo nikakamilisha tungo ambayo inaanza kwa kusema:

”Allaah, Mtukufu, ametakasika kutokamana na mapungufu. Anahimidiwa kwa upole na baada ya ujuzi Wake.”

Kwa ajili hiyo nitapanga na kuweka wazi mkusanyiko huo. Namuomba Allaah msaada, Yeye ndiye anatutosha na ndiye mbora Mwenye kutegemewa.

Allaah (Ta´ala) amesema – na ni nani mkweli zaidi kuliko Allaah:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[1]

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ

“Yeye ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita na ‘Arshi Yake ikawa juu ya maji.”[2]

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]

الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا

”Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha akalingana juu ya ‘Arshi; Mwingi wa rehema; basi ulizia kuhusu khabari Zake.”!”[4]

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ

”Kisha akalingana juu ya mbingu iliali ni moshi, akaziambia pamoja na ardhi: ”Njooni kwa kutaka au kwa lazima. Zikasema: ”Tumekuja hali ya kuwa tumetii.”[5]

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا

“Yeye ndiye ambaye amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini.”[6]

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

“Yeye ndiye ambaye amekuumbieni yote yaliyomo ardhini kisha akazielekea mbingu na akazitimiza mbingu saba. Naye juu ya kila jambo ni Mjuzi.”[7]

يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

”Anayaendesha mambo kutoka mbinguni mpaka ardhini, kisha inapanda Kwake katika siku ambayo kipimo chake ni sawa na miaka elfu katika yale mnayoihesabu nyinyi.”[8]

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake linapanda neno zuri na tendo zuri hulitukuza.”[9]

يَا عِيسَى إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

“Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.”[10]

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

”Bali Allaah alimnyanyua Kwake. Allaah ni Mwenye nguvu kabisa, Mwenye hekima wa yote.”[11]

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu.”[12]

مِّنَ اللَّـهِ ذِي الْمَعَارِجِ تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ

“… kutoka kwa Allaah Mwenye njia za kupandia. Malaika na Roho wanapanda Kwake katika siku kadiri yake ni miaka elfu khamsini.”[13]

يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَ أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا

“Ee Haamaan nijengee mnara ili nifikie njia; njia za mbinguni ili nimchungulie Mungu wa Muusa, kwani hakika mimi namdhania ni mwongo.”[14]

Yapo maandiko mengine kama hayo mengi ndani ya Qur-aan Tukufu – kimetakasika cheo Chake na amekutuka Mzungumzaji Wake.

[1] 7:54

[2] 11:7

[3] 20:5

[4] 25:59

[5] 41:11

[6] 02:29

[7] 2:29

[8] 32:5

[9] 35:10

[10] 3:55

[11] 4:158

[12] 67:16-17

[13] 70:3-4

[14] 40:36-37

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 79-80
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy