Ni jambo limesuniwa kwa waislamu wote kujipinda katika aina mbalimbali za ´ibaadah kaitka mwezi huu mtukufu ikiwa ni pamoja na swalah zinazopendeza, kusoma Qur-aan kwa mazingatio na kuielewa, kusema ”Subhaan Allaah”, ”Laa ilaaha illa Allaah”, ”Alhamdulillaah”, ”Allaahu Akbar” na ”Astaghfiru Allaah” kwa wingi, kuomba du´aa zilizowekwa katika Shari´ah, kuamrisha mema, kukataza maovu, kulingania kwa Allaah, kuwafariji mafukara na masikini, kujitahidi kuwatendea wema wazazi, kuunga kizazi, kuwakirimu majirani, kuwatembelea wagonjwa na sampuli nyenginezo za mambo ya kheri. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Allaah huangalia namna ya kushindana kwenu ambapo akajifakharisha juu yenu mbele ya Malaika. Muonyesheni kheri kutoka katika nafsi zenu. Hakika mwangamivu ni yule aliyenyimwa ndani yake rehema za Allaah.”
Imepokelewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
”Mwenye kujikurubisha humo kwa jambo la kheri, basi anakuwa ni kama ambaye ametekeleza faradhi katika isiyokuwa hiyo [Ramadhaan], na mwenye kutekeleza humo faradhi, basi anakuwa kama ambaye ametekeleza faradhi sabini katika isiyokuwa hiyo [Ramadhaan].”
Zipo Hadiyth na Aathaar nyingi zinazofahamisha juu ya kusuniwa kushindana katika mambo mbalimbali ya kheri ndani ya mwezi huu Mtukufu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Min A´maal Ramadhwaan, uk. 03
- Imechapishwa: 29/03/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
