Swali: Ni yepi maoni yako juu ya hukumu ya upigaji picha ambao janga lake limeenea na watu kujishughulisha? Tunaomba jawabu lenye kutosheleza juu ya zile zinazoruhusiwa na zile zilizoharamishwa.

Jibu: Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee ambaye hakuna Mtume mwengine baada yake.

Amma ba´d:

Kumepokelewa Hadiyth nyingi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika vitabu ambavyo ni “as-Swihaah”, “al-Masaanid” na “as-Sunan” zinazofahamisha uharamu wa kuchukua picha kila kiumbe chenye roho. Ni mamoja kiumbe hicho ni binadamu au chengine, mapazia yenye picha, maamrisho ya kutweza picha, kulaaniwa kwa wenye kuchukua picha na kubainisha kuwa ndio watu wenye adhabu kali siku ya Qiyaamah.

Nitakutajia baadhi ya Hadiyth ambazo ni Swahiyh zilizopokelewa juu ya maudhui haya, baadhi ya maneno ya wanazuoni juu yake na nitakubainishia kilicho sahihi katika suala hili – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jawaab al-Mufiyd fiy Hukm-it-Taswwiyr kutoka katika Majmuu´-ul-Fataawaa (04/210)
  • Imechapishwa: 24/03/2022