00. Utangulizi wa kitabu “Thalaathat-il-Usuwl”

Hiki ni kijitabu muhimu na cha ´Aqiydah kilichoandikwa na Imaam na Shaykh Abu ´Abdillaah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab bin Sulaymaan at-Tamiymiy al-Hanbaliy. Alikuwa ni imamu mwenye kujulikana na mujadidi aliyeishi katika nusu ya mwisho ya karne ya 1100 ambapo ´Aqiydah ya Kiislamu ilikuwa imeharibika. Allaah amerehemu na amtunuku thawabu tele.

Alizaliwa 1115 na akafariki 1206. Maisha yake yalikuwa yamejaa kheri, kulingania katika dini ya Allaah, mafundisho, maelekezo na subira juu ya mazito.

Kupitia yeye Allaah amewaokoa waja na miji katika kisiwa cha Kiarabu. Baada ya hapo Da´wah yake ikaenea nje ya kisiwa cha Kiarabu na ikafika mpaka Shaam, Misri, ´Iraaq na India na kwa sababu ya walinganizi waliyofikisha elimu yake na wakahamia katika miji hiyo na kwa sababu vilevile ya wafanya biashara wa vitabu na vitabu vilivyoenezwa kutoka kwake (Rahimahu Allaah), wafuasi wake, wanusuraji wake na waliokuja wenye kulingania katika dini ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 05
  • Imechapishwa: 15/10/2016