00. Hakuna kitabu mfano wa “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah”

Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na mwenye kufuata uongofu wake.

Ama baada ya hayo;

Kitabu hichi chenye thamani kikubwa kwa jina “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” kimeandikwa na Shaykh-ul-Islaam Abul-´Abbaas Ahmad bin ´Abdil-Haliym bin ´Abdis-Salaam bin Taymiyyah al-Harraaniy (Rahimahu Allaah). Mtu huyu alikuwa ni Imaam, baba na babu yake pia walikuwa vivyo hivyo. Wote walikuwa ni maimamu wa elimu na uongofu. Alizaliwa mwaka wa 661 na akafariki mwaka wa 728. Ina maana aliishi miaka 68.

Aliwakusanyia ´Aqiydah hii watu wa Waasitw upande wa ´Iraaq. Imeitwa kuwa ni “al-Waasitwiyyah” kwa sababu wameandikiwa wao. Kama ambavyo ana kitabu chake kingine kinachoitwa “al-Hamawiyyah” kwa sababu waliandikiwa watu wa Hamaah, kingine kinachoitwa “at-Tadmuriyyah” kwa sababu aliwaandikia watu wa Tadmur. Ni vitabu vitukufu. “at-Tadmuriyyah” ni kitabu kitukufu ijapokuwa ni kikubwa kuliko hiki. Vivyo hivyo “al-Hamawiyyah” ndani yake mna nukuu nyingi kutoka kwa maimamu wa Salaf (Rahimahumu Allaah). Kuhusiana na kitabu hichi “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” ni mukhtaswari, chenye faida na kilichokusanya. Hatujui kama kuna kitabu mfano wake miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa na watu kutokamana na ufupi wake lakini hata hivyo kimekusanya ´Aqiydah ya Salaf. Ametumia (Rahimahu Allaah) ibara ambazo ni za wazi na usulubu bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 8
  • Imechapishwa: 31/05/2023