Swali: Ni sahihi ziada inayosema:

إنك لا تخلف الميعاد

“Hakika wewe hauendi kinyume na ahadi Yako”?

katika Dhikr inayosomwa baada ya adhaana?

Jibu: Ziada hii ni kitu wanachuoni wa Hadiyth wametofautiana. Wako waliosema waliosema kuwa haikuthibiti kutokana na unyonge wake. Kwa sababu wengi waliopokea Hadiyth hawakupokea neno hili. Sehemu inapelekea kwamba haikufutwa. Kwa sababu sehemu yenyewe ni ya du´aa na sifa. Kitu kinachokuwa kwa njia hiyo basi haifai kukifuta kwa sababu ni chenye kufanyiwa ´ibaadah.

Wanachuoni wengine wakasema kuwa cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh na kwamba inasemwa na kwamba haipingani na nyenginezo. Miongoni mwa wenye kuonelea kwamba ni sahihi ni Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz. Amesema kwamba cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh kwa vile imepokelewa na al-Bayhaqiy kwa cheni ya wapokezi ambayo Swahiyh[1].

[1] (01/410). Tazama ”Fataawaa al-Lajnah” (06/88) na ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (10/364) ya Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 286-287
  • Imechapishwa: 29/04/2020