Download

120-

اللّهُـمَّ إِنِّي عَبْـدُكَ، ابْنُ عَبْـدِكَ، ابْنُ أَمَتِـكَ نَاصِيَتِي بِيَـدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤكَ، أَسْأَلُـكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ، سَمَّـيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أِوْ أَنْزَلْتَـهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ عَلَّمْـتَهُ أَحَداً مِنْ خَلْقِـكَ، أَوِ اسْتَـأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الغَيْـبِ عِنْـدَكَ، أَنْ تَجْـعَلَ القُرْآنَ رَبِيـعَ قَلْبِـي، وَنورَ صَـدْرِي، وجَلَاءَ حُـزْنِي، وذَهَابَ هَمِّـي

!Ee Allaah! Hakika mimi ni mja Wako, mwana wa mja Wako, mwana wa mjakazi Wako, utosi wangu uko mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni adilifu kwangu unihukumu kwayo, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako; ulilojiita kwalo Mwenyewe, uliloliteremsha katika Kitabu Chako, ulilomgunza nalo yoyote katika viumbe Vyako, ulilolificha katika elimu ya ghaibu Kwako: nakuomba uifanye Qur-aan kuwa ni uhuisho wa moyo wangu, nuru ya kifua changu na ufumbuzi wa  huzuni yangu.”[1]

121-

اللّهُـمَّ إِنِّي أَعْوذُ بِكَ مِنَ الهَـمِّ وَالْحُـزْنِ، والعًجْـزِ والكَسَلِ والبُخْـلِ والجُـبْنِ، وضَلْـعِ الـدَّيْنِ وغَلَبَـةِ الرِّجال

”Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na hamu na huzuni, kushindwa na  uvivu, ubakhili na woga, uzito wa deni na kushindwa na watu.”[2]

[1] Ahmad (01/391). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

[2] al-Bukhaariy (07/158). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba kwa wingi du´aa hii.” Tazama “al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (11/173). Itakuja katika uk. 89, nambari (137).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 29/04/2020