Zakaat-ul-Fitwr ya mfanyakazi muislamu nyumbani

Swali: Je, ni lazima kwa mfanya kazi wa nyumbani kutoa Zakaat-ul-Fitwr?

Jibu: Ni wajibu kwake kutoa Zakaat-ul-Fitwr kwa sababu ni muislamu. Lakini je, ni lazima kwake kujitolea Zakaat-ul-Fitwr mwenyewe au ni lazima kwa watu wa nyumbani kwake kumtolea? Msingi ni kwamba yeye mwenyewe ndiye anatakiwa kujitolea. Lakini watu wa nyumbani kwake wakimtolea hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/263)
  • Imechapishwa: 21/06/2017