Zakaat-ul-Fitwr kwa waliokufa katika mwishoni mwa Ramadhaan

Swali: Kuna mtu amekufa siku ya mwisho ya Ramadhaan kabla ya kuzama kwa jua na mwingine amekufa baada ya kuzama kwa jua. Ni yupi kati ya hao wawili ambaye analazimika kutoa Zakaat-ul-Fitwr?

Jibu: Ambaye amekufa kabla ya kuzama kwa jua usiku wa kuamkia ´Iyd-ul-Fitwr halazimiki kutoa Zakaat-ul-Fitwr. Kwa sababu zakaah inawajibika pale linapozama jua katika usiku huo ilihali yeye amekufa kabla ya kuwajibika. Ambaye amekufa baada ya kuzama kwa jua ni lazima kwake kutoa Zakaat-ul-Fitwr. Kwa sababu amekufa baada ya kuwajibika.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillah bin Baz

´Abdul-´Aziyz Aalush-Shaykh

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (20514)
  • Imechapishwa: 13/05/2020