Swali: Inajuzu kwa yale mashirika ya Zakaat-ul-Fitwr kununua chakula katika ile siku ya kwanza ya Ramadhaan kisha kukigawanya kwa mafukara katika mwisho wa mwezi pamoja na kuzingatia kwamba wale watoaji hunuia pale inapotolewa. Je, inajuzu kuitoa kabla ya kunuia?

Jibu: Wakati wa kutoa Zakaat-ul-Fitwr ni baada ya kuandama mwezi wa Shawwaal mpaka kabla ya swalah ya idi. Inajuzu kuitanguliza siku moja au mbili kabla ya swalah ya ´iyd. Yule mtoa zakaah anapaswa kujitolea yeye mwenyewe na wale anaowasimamia na kuwapa wale wenye kuiistahiki. Pia anaweza kuwakilisha mtu anayemwamini kumtolea nayo katika wakati wake maalum. Kwa sababu ni haki ya lazima ilio juu ya dhimma yake. Haijuzu kuchukulia wepesi katika kuitoa wala kutegemea mashirika yanayochukulia jambo hilo wepesi.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillah bin Baz

´Abdul-´Aziyz Aalush-Shaykh

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (20514)
  • Imechapishwa: 13/05/2020