Wingi na uchache wa damu ya nifasi na hukumu yake

Swali: Anapozaa mwanamke, ipi hukumu ya damu ya uzazi? Je, hukumu yake ni kama nifasi au hedhi? Na upi muda wake mwingi na uchache wake?

Jibu: Baada ya kutoka mtoto damu itokayo ni nifasi hata ikiwa ni ndogo. Hukumu yake ni nifasi. Ni juu yake kusubiri mpaka atapotwaharika. Na wala asinuie arubaini kwa kuwa huu ni wingi wa damu ya nifasi, siku arubaini. Akitwaharika kabla ya siku hizo baada ya siku ishirini au mwezi, atakoga na kuswali na kufunga na anakuwa halali kwa mume wake. Damu yake ikiendelea ataacha kuswali na kufunga na si halali kwa mume wake mpaka zifike siku arubaini. Zikifika siku arubaini, nifasi yake imekwisha. Ataswali, atafunga na ni halali kwa mume wake hata kama damu itakuwa bado yamtoka, kwa kuwa… [sauti haiko wazi]. Kwa kuwa [damu ya] nifasi wingi wake ni siku arubaini. Ikizidi siku hizo ni damu ya ugonjwa. Ataswali na kufunga baada ya kukoga na ni halali kwa mume wake na ajihifadhi [kwa kitu] sehemu ya tupu… Ama akitwaharika chini ya siku hizo, akatwaharika [baada ya] siku ishirini, kumi na tano au siku thelathini nk, atakoga, kuswali, kufunga hata kama ni kati kati ya siku arubaini. Na ni halali kwa mume wake. Mwanamke huyu atatawadha kwa kila swalah unapoingia wakati wake na hukumu yake ni kama mwenye istihaadha, na mwenye kutokwa hovyo na mikojo na mgonjwa. Atapopata shida, anaweza kujumuisha dhuhr na ´aswr pamoj; na akajumuisha maghrib na ´ishaa pamoja kwa ajili ya damu. Katika hali hii hukumu yake ni kama kwenye istihaadha kwa kuwa sio nifasi; mpaka itapokatika.

Check Also

Kufanya sherehe inapoisha nifasi ya mwanamke siku arubaini

Swali: Ipi hukumu ya “al-Arba´iyniyyah” yaani mwanamke mwenye nifasi damu yake inapokatika na akatwahirika damu …