Watu wenye kuamini mazingira ni wenye ukafiri mbaya zaidi

Swali: Tunafanya vikao na vijana Ufaransa ambao hawaamini kuwa Allaah ndiye Mwenye kuumba wala Mwenye kuruzuku wala kufufuliwa kama wakomunisti. Je, wao ni washirikina?

Jibu: Hili ni kubwa zaidi kuliko shirki. Huu ni ukanamungu. Ni ukafiri mkubwa kushinda ukafiri wa Quraysh. Wao ni wakanamungu. Hawamwamini Mola, Muumbaji na Mruzukaji. Ukafiri wao ni mkubwa zaidi. Wao wanaona:

إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا

“Hakuna chochote isipokuwa tu uhai wetu wa duniani; tunakufa na tunahuika.”[1]

[1] 23:37

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 56
  • Imechapishwa: 27/06/2019