Swali: Sisi tuna baadhi ya wapotevu wanaojinasibisha na Salafiyyah. Kuna ambao wanamtetea ´Aliy al-Halabiy na jumuiya ya Ihyaa´ at-Turaath na wanatahadharisha kuhudhuria semina itayoendeshwa na Shaykh na Dr. Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy na Shaykh ´Abdullaah bin Salfiyq Dammaam na Hafr-ul-Baatin. Unanasihi nini?

Jibu: Wale wanaomtetea al-Halabiy, watu mfano wake na Ihyaa´ at-Turaath hawajui Salafiyyah ni kitu gani. Nyoyo zao zina maradhi. Hili linatiliwa nguvu na kule kutahadharisha kwao semina za Salafiyyuun kama ya Shaykh Muhammad bin Haadiy, al-Bukhaariy na ´Abdullaah bin Salfiyq. Nyoyo zao zina maradhi na ni wajibu kwao kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Nyoyo zao zina maradhi. Hawajui Salafiyyah ni kitu gani. Wangelikuwa wanaielewa Salafiyyah basi wasingeliwatetea watu hawa. Ni upotevu kiasi gani walionao! Ni mabalaa gani walionayo! Nimeandika mujaladi kuhusu al-Halabiy ambapo ndani yake nimebainisha misingi yake. Maneno na raddi zangu zote zinahusiana na upotevu wake. Ni juu ya Salafiyyah kushaji´isha semina za Salafiyyah na watahadhari kweli kweli na semina za Ahl-ul-Bid´ah na semina za wenye maradhi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=_4BmLfjybbg
  • Imechapishwa: 04/02/2017