Wasiwasi wakati wa kutawadha


Swali: Baada ya kumaliza kutawadha huhisi kuwa natokwa na matone ya mkojo. Je, ni lazima kwangu kurudi kutawadha kwa kuzingatia kwamba kila ninaporudia kutawadha nahisi hisia zilezile? Nifanye nini?

Jibu: Hisia hizi za muulizaji baada ya kutawadha huzingatiwa ni katika wasiwasi wa shaytwaan. Kwa hivyo si lazima kurudia kutawadha. Bali kilichowekwa katika Shari´ah kwake ni yeye kupuuzia jambo hilo na ahesabu kuwa wudhuu´ wake ni sahihi na haujachenguka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati alipoulizwa juu ya mtu ambaye anahisi kitu ndani ya swalah yake ambapo akasema:

“Asiondoke mpaka asikie sauti au ahisi harufu.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Isitoshe shaytwaan ni mwenye kupupia kuziharibu ´ibaadah za muislamu kukiwemo swalah, wudhuu´ na nyenginezo. Kwa hivyo ni lazima kumpiga vita na kutonyenyekea wasiwasi wake. Sambamba na hilo mtu amwombe Allaah ulinzi kutokamana na uchochezi na vitimbi vyake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/124)
  • Imechapishwa: 21/08/2021