Wasiwasi wa Shaytwaan katika kheri


Tambua ya kwamba shaytwaan anaweza kukujia pale unapotaka kufanya matendo ya kheri na akakwambia ya kwamba unachokifanya ni kwa ajili unataka kujionyesha ili akusitishe. Usijali hili na wala usimtii. Fanya matendo hata kama atakwambia kuwa unafanya hivo kwa ajili ya kutaka kujionyesha au kutaka kusikika. Kwa sababu, lau mtu atakuuliza “Je, wewe unafanya hili kwa ajili ya kutaka kujionyesha na kusikika?” Jibu itakuwa hapana. Hivyo basi, wasiwasi huu ambao shaytwaan ameuingiza ndani ya moyo wako usiujali. Fanya matendo ya kheri na wala usisemi kuwa mimi pengine najionyesha na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/16)
  • Imechapishwa: 26/12/2017