Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni ajabu iliyoje kuona wafuasi wa ´Abdullaah bin Sabaa´, wafuasi wa waabudu moto, washirikina wenye kuabudu masanamu, vifaranga vya Jahmiyyah na Fir´awn wakawa ni wajuzi zaidi juu ya Allaah kuliko Muusa mwana wa ´Imraan, juu ya mambo ambayo ni muhali Kwake, ambalo lilikuwa la wajibu kwake na kumtakasa kukubwa zaidi kuliko yeye [Muusa]!”

Muusa (´alayhis-Salaam) anaonelea kujuzu kuonekana kwa Allaah na ndio maana akawa amemuomba kumuona. Wao wanasema kuwa haijuzu kwa Mola Wetu (Tabaarak wa Ta´ala) kuonekana. Je, wao ni wajuzi zaidi kuliko Muusa? Yaani hawa waabudu moto, wafuasi wa ´Abdullaah bin Sabaa´ na wapotevu na wajinga wengine ni wajuzi zaidi juu ya Sifa za Allaah na Sifa ambazo ni kamilifu kumshinda Muusa? Je, wao wanamtakasa Allaah zaidi kuliko Mitume wanavyomtakasa? Allaah amemtakasa Muusa na Mitume kunena juu ya Allaah yale wasiyoyajua.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 27/08/2020