Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuwatenga mbali wa wanawake na wanaume mpaka sehemu za kufanyia ´ibaadah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safu bora za wanawake ni zile ziliko nyuma na ovu zake ni zile zilizoko mbele.”

Kwa nini? Kwa sababu zile safu wanawake zilizoko nyuma ziko mbali zaidi ya wanaume. Kwa ajili hiyo ndio maana zikawa bora zaidi. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotoa Tasliym kutoka katika swalah basi anasubiri kidogo na hatoki nje mpaka kwanza waondoke wanawake kabla ya wao kuchanganyikana na wanaume.

Vilevile kumepokelewa Hadiyth inayomkataza mwanamke kutembea katikati ya barabara ili asije kuchanganyikana na wanaume, hili ni jambo linalotambulika katika Shari´ah. Hakuna ambaye halijui isipokuwa yule ambaye si msomi wa yale yaliyoandikwa na wanachuoni kuhusu jambo hilo.

Kwa ajili hii nasema kwamba mtu anapaswa kuikoa nafsi yake yeye na familia yake kutokamana na Moto wa Jahannam kwa kuwaelekeza wanawake juu ya yale wanayopasa kufuata kujiheshimu, kuwa na haya, kujisitiri, kujitenga mbali na kuchanganyikana na wanaume. Bali wanatakiwa vilevile kujiepusha na kuwazungumzisha wanaume kwa njia ambayo inapelekea katika fitina. Kwa ajili hii Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

“Msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika.”[1]

[1] 33:32

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1449
  • Imechapishwa: 31/12/2019