Wanawake kuzipamba sauti zao za Qur-aan mbele ya mwalimu wa kiume

Swali: Dada huyu anauliza ni ipi hukumu ya wanafunzi wa kike kuremba sauti zao wakati wa kusoma Qur-aan mbele ya mwalimu wa kiume katika chuo kikuu pamoja na kuwa mwanamke hakutakiwa kufanya hivo?

Jibu: Sionelei apambe sauti yake. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

“Hivyo basi msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika.”[1]

Kule mwanafunzi wa kike kusoma Qur-aan kwa utaratibu ipasavyo na utungo na kwa kuremba sauti kunakhofiwa fitina. Inatosha kwake kusoma Qur-aan kisomo cha kawaida.

[1] 33:32

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/927
  • Imechapishwa: 04/12/2018