Swali: Je, inajuzu kwa wanawake kuwatahadharisha watu na vitabu vya Sayyid Qutwub?

Jibu: Ikiwa ni wanafunzi wanawake watahadharishe kwa kutaja vitabu vya Sayyid Qutwub, ad-Dhwilaal (al-Qur-aan), al-Adaalah (al-Ijtimaa´iyyah) na mfumo wake.

Himdi zote ni za Allaah kuona hivi karibuni Muhammad Qutwub ametangaza utahadharisho (wa Sayyid Qutwub) juu ya vitabu vyote alivyoandika kabla ya adh-Dhwilaal. Mashaa Allaah! Yaani baada ya miaka thalathini arubaini ndio unakuja na kusema kuwa ametahadharisha vitabu hivi baada ya vijana kuangamia! Ni ghush kubwa ilioje hii. Mtu huyu anazingatiwa kuwa ni “Imaam” kwa vijana. Zaidi ha hayo, ametoa idhini ya kuchapisha vitabu vyote hivi na kumpiga vita kila yule mwenye kuvichapisha bila ya idhini yake. Ni mamilioni ya mapesa ya watu wangapi yamechukuliwa pasina haki kwa gharama za ´Aqiydah na vijana wa Ummah. Kwa nini aliwafanya Maswahabah kuonekana ni watu wasiokuwa na maana kwa vijana wa Ummah? Wivu wao kwa Sayyid Qutwub ni mkubwa kuliko wivu wao kwa Mitume, Maswahabah na wanachuoni wa Uislamu. Ninaapa kwa Allaah juu ya hili. Kwa sababu wamefungamanishwa na mfumo wake wa Tafiyr ya ki-Khawaarij, ambapo Bid´ah zake zote, upotevu na mambo yote ya khatari yameonekana kutokuwa na maana kwao.

Kwa ajili hiyo ni wajibu vitabu hivi virudiwe. adh-Dhwilaal imejaa upotevu. adh-Dhwilaal imejaa upotevu. Kadhalika kitabu chake “at-Taswiyr al-Fanniy”, sijaona mtu yeyote mwenye jeuri na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume kama mtu huyu. Kitabu chake kimejengeka juu ya misingi mibaya, upotevu, ujeuri na kukitia mitihanini kwa kukitia aina mbali mbali za muziki, sinema, maigizo na kadhalika. Huku ni kuifedhehesha Qur-aan kwa njia isiyokuwa na mfano katika historia, kisha wakati huo huo anajisifia na kusema kuwa amefikia mambo ambayo hakuna yeyote aliyeyafikia hapo mwanzoni.

Wengi katika watu wajinga hawawezi kufikiria upotevu huu aliouweka katika Qur-aan kwa uongo. Wengi katika watu wajinga wanakiheshimu Kitabu cha Allaah na wanajua kuwa kimesalimika na mambo haya, wakati yeye anajua.

at-Taswiyr al-Fanniy kimetoka kabla ya adh-Dhwilaal, kwa nini hamkukitahadharisha? Bali alijadiliana na mwanafunzi mmoja, kabla ya mwaka wa 1400 Hijry, kuhusiana na kitabu hichi, pamoja na hivyo baada ya miaka ishirini kitabu hichi bado kinaenezwa na kuchapishwa, halafu baada ya hapo unakuja na kusema kwamba kaka yako alitahadharisha kitabu hichi? Ni uongo sampuli gani, njama na kampeni kwa Ummah kama huu? Amekuwa ni Imaam mkubwa, ni jambo linaloonesha jinsi vijana ambao bado ni wachanga kielimu na wapumbavu wa akili walivyoangamia.

Mtu huyu ameufanyia ghush Ummah na kuusaliti. Baada ya kueneza vitabu hivi potevu katika mashariki na magharibi kwa lugha mbalimbali na Ummah ukawa umeshaangamia, ndio anakuja na kusema Sayyid Qutwub amevitahadharisha. Kwa nini hamkukiri kuwa kuna upotevu katika adh-Dhwilaal? Namna hii ndivyo ilivyo Da´wah yao imejengeka juu ya ghush, talbisi, wadogo kiumri na ni wapumbavu wa akili.

Ni wajibu tuelekeze na kuwafanya wakulie katika daraja ya uongofu. Kwa sababu amekulia juu ya Suufiyyah na Tijaaniyyah na yeye akawalea vijana wa Ummah juu ya ukandamizwaji na ufuataji upofu na upotevu n.k. Kwa ajili hiyo ndio maana wako sehemu ambapo inafanana sana na watumwa wakandamizwaji kwa hawa ambao wanawaamrisha kama wanyama wasiokuwa na akili.

Hivi sasa watu wamepagawa juu ya Takfiyr ya Sayyid Qutwub kana kwamba ni wanaume wehu. Wanatumia matusi ya Sayyid Qutwub kuwatukana Maswahabah, Mitume na hawana wivu wa hilo na wala hawarudi hilo. Endapo wewe unawakumbusha kwa haki na kuwatahadharisha, hawakubali hilo. Akili zako ziko wapi? Ndio maana uko katika wale ambao ni wadogo kiumri na wapumbavu wa akili wasiokuwa na Dini na tabia. Ni wajibu tuzilee nafsi zetu katika upeo wa juu, kujiokoa na wakati huo huo kujitahidi kusaidizana sisi kwa sisi kujiokoa.

Mimi binafsi sijui kitu ambacho ni khatari zaidi kama vitabu vya Sayyid Qutwub na wafuasi wake. Katika kisiwa hichi cha kiarabu fitina ya Musaylimah na wingu la majira ya joto lilikuja na kuondoka. Lakini fitina hii khabithi imechukua mizizi kwa ndani kabisa katika ardhi na imeingia katika nchi hii ya Tawhiyd. Vijana wa nchi hii ni Qutbiyyuun ambao wamekuwa ni wenye kueneza fitina hii ulimwenguni na ni pigo la Uislamu ambalo halikuwahi kuonekana hapo mwanzoni. Ninasema haya pasina kupetuka mipaka bali ndio uhakika wa mambo.

Allaah Ameitengeneza nchi hii na kuisafisha kupitia mikono ya watengenezaji, Da´wah ya Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ambaye alisafisha mambo yote ya shari, fitina, Shirki, uchawi, uongo na udanganyifu. Hivi sasa amewashughulisha vijana na siasa, uchawi, ukuhani ambao umejengeka juu ya uongo na uovu na kwamba sisi wote ikiwa ni pamoja na jamii yetu [ya Kiislamu] ni makafiri. Hii ni kwa sababu wanasoma vitabu vya Sayyid Qutwub ambavyo vinaikufurisha jamii ya Kiislamu. Hata hivyo wana Taqiyyah, uongo na unafiki. Kwa sababu vipi mtu ambaye amekinaika na vitabu vya Sayyid Qutwub na kuvitetea asiamini yaliyomo ndani yake?

Mimi hivi sasa napigana vita kwa kumraddi ar-Rafdhw. Ikiwa mtu atasema kuwa hawa sio Raafidhwah, lakini anaeneza vitabu na kuchapisha vitabu vyao kwa lugha mbali mbali ambavyo vinaenezwa ulimwenguni. Vipi utamchukulia mtu huyu Raafidhwiy au nini? Kadhalika mtu ambaye anaeneza na kukuza vitabu vya Sayyid Qutwub, anaamini yale yaliyomo katika I´tiqaad mbovu na fikira chafu na khaswa khaswa ikiwa anavichapisha na kuvitetea.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=B5KwBd9WGj8
  • Imechapishwa: 22/04/2015