Swali: Kuna mtu anaeneza maovu ya mtawala wa waislamu kwa hoja eti anabainisha Shari´ah ya Allaah juu ya hilo na kwamba anazungumza neno la haki. Ni ipi hukumu ya kitendo kama hichi?

Jibu: Hivi ndivo wafanyavyo Khawaarij. Haijuzu kufanya hivi. Mtawala akifanya kosa basi unatakiwa kumnasihi kwa siri. Usiyaonyeshe haya kwa watu. Mnasihi kwa siri. Akikubali ni vizuri. Akikataa utakuwa umetekeleza wajibu wako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 10/09/2018