Sisi tunasema kukipatikana hukumu kutoka kwa mwanachuoni ya kwamba mtu fulani ni katika Ahl-ul-Bid´ah na mwanachuoni huyu anajulikana [kuaminika] kwa kazi hii [Jarh wa Ta´diyl] na hatujui uhalifu wowote kwake, hatusemi mpaka kwanza tuthibitishe wenyewe au kujionea wenyewe. Badala yake tunachukua kauli ya mwanachuoni huyu kwa kuwa hatuna kipingamizi. Huu ndio mfumo wa Salaf. Imaam Ahmad alikuwa akisema fulani ni katika Ahl-ul-Ahwaa´, basi kunasemwa kuwa ni katika Ahl-ul-Ahwaa´ na hakujitokezi mwenye kipingamizi.

Endapo wanachuoni wawili ambao wote wanakubalika watatofautiana juu ya mtu fulani, basi sisi tutatazama. Ikiwa yule mwenye kumkosea anazungumzia kitu anachokijua fika na upande mwingine yule mwenye kumsifu anazungumzia kitu cha zamani na hajui hali yake, basi sisi hapana kunakuja kanuni isemayo:

“Yule mwenye ujuzi ana hoja juu ya yule asiyejua.”

Hili pia linatumika kinyume chake. Ikiwa yule mwenye kukosoa anategemea mambo yaliyopita. Kwa mfano mtu huyu ambaye wewe unamkosoa alikuwa ni Hizbiy na mtu wa Bid´ah hapo mwanzoni na upande mwingine yule mwenye kukosoa anazungumza kwa elimu anayoujua fika ya hali yake ya sasa na kwamba mtu huyu ameshajirudi. Basi katika hali hii tunasema kanuni ile ile:

“Yule mwenye ujuzi ana hoja juu ya yule asiyejua.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda “as-Salafiyyah wa Hayaatah” https://www.youtube.com/watch?v=Jq9DehxRLE8
  • Imechapishwa: 16/11/2014