Kuna watu wanaojinasibisha na Salafiyyah ilihali hawashikamani bara bara na misingi yake. Hilo ni kwa sababu ima anataka kueneza madhehebu yake. Yeye anaona kuwa jamii inakubali Salafiyyah au wanachuoni Salafiyyuun wameeneza mfumo wa Salaf na imepata nguvu, sasa na yeye anajiita “Salafiy”, lakini wakati huo huo ukitazama sifa na tabia yake hutopata isipokuwa utaona Hizbiyyah. Hili watu wanatakiwa kulizingatia. Kinachozingatiwa sio kujiita, bali kinachozingatiwa ni uhakika wa mambo.

Upande mwingine kuna ambao wanajinasibisha na Salafiyyah ili wawadanganye wenye kuwasikiliza. Ukiona anatumia neno “Salafiy”, basi kuwa  na tahadhari! Mfano wa watu unatakiwa kuwa na tahadhari ni kama wale wanaojiita “as-Salafiyyah al-Jihaadiyyah”, wengine ni wale wenye kujiita “as-Salafiyyah wal-Jihaad”, “as-Salafiyyah al-Kuwayt”, “as-Salafiyyah as-Su´udiyyah”, “as-Salafiyyah al-Ordon”, “as-Salafiyyah al-Miswriyyah”.

Salafiyyah ni moja na haoingezwi juu yake kitu. Ukiona Salafiyyah yenye kuongezwa juu yake vijineno na yenye kujibagua, basi kuwa  na tahadhari. Salafiyyah hiyo ina kasoro.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda “as-Salafiyyah wa Hayaatah” https://www.youtube.com/watch?v=Jq9DehxRLE8
  • Imechapishwa: 16/11/2014