“Wanachuoni hawa kazi yao ni kusengenya watu tu”


Swali: Leo kuko ambao wanatahadharisha Shaykh Rabiy´ na Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy na wanasema ya kwamba watu hawa wanajishughulisha tu na kusengenya na kuwaongelea watu na wala kamwe hawazungumzii kuhusu Tawhiyd. Vipi tutawaraddi?

Jibu: Tunawaraddi kwa sentesi yao ya mwisho. Shaykh Muhammad [al-Jaamiy] karibu maneno yake yote ni kuhusu Tawhiyd. Shaykh Rabiy´ karibu maneno yake yote ni kuhusu kuitetea ´Aqiydah na Sunnah. Allaah amrehemu aliyetangulia na amuwafikishe aliyebaki. Vitabu vyao vinathibitisha hilo. Mithali inasema ya kwamba maji yanamfichukua mwenye kudai ya kwamba anajua kuogelea ilihali ni mwongo.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=141264
  • Imechapishwa: 15/05/2018