Swali: Baadhi yao wanaeleza kuwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz na Shaykh Ibn ´Uthaymiyn wamejuzisha kuingia kwenye mabunge kama haya ili kuepuka madhara makubwa. Wanaonelea kuwa Waislamu wakiwaacha watende madhambi na wazushi wakashika nyanja kama hizi wao ndio watakuwa wengi na hivyo kutakuwa madhara makubwa kwa Waislamu. Kwa mujibu wao kuingia kwenye bunge inajuzu ili kuepuka madhara makubwa.

al-Albaaniy: Haya ni ambayo wanafikiria na natamani fikira zao ingelikuwa ni ukinaishaji. Lakini kwa masikitiko makubwa uhalisia unatuonyesha tangu al-Ikhwaan al-Muslimuun walipozua Bid´ah ya kuingia bungeni kwa lengo hili hili hatukuona faida yoyote kabisa na bunge. Walichoweza kufanya tu ni kusaidia bunge na kuhakikisha sheria zao zinazokwenda kinyume na Shari´ah zinatekelezwa.

Sipingi kuwa kunaweza kuwa faida, lakini faida hii sio muhimu. Ni kama mfano wa maradhi yenye kuonyesha dalili kwenye mwili na yanapunguzwa kwa vidonge vya maumivu. Pamoja na hivyo ni nadra. Ama kusema kuwa vitatibu ugonjwa kikamilifu, uhalisia wa mambo ni dalili kubwa ya kwamba mambo sivyo. Ni mara ngapi tutakuja na madai kama haya wakati makundi mengi ya Kiislamu yalijaribiwa kwa furaha kwa makumi ya miaka? Hivi sasa tuko kwenye jaribio jipya. Inatosha kwa mtu akapata funzo. Ndio maana ninawanasihi kutafuta elimu:

“Allaah Kumwongoza mtu mmoja kupitia kwako, ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”

Swali: Hapo mwanzoni umesema kuwa watu hawa wanaingia [bungeni] ili kubadilisha lakini wanabadilika wao wenyewe.

al-Albaaniy: Wanabadilika, ndio. Ni kitu kimeshuhudiwa. Baadhi ya ndugu zetu Kuwait wameingia [bungeni] wakiwa na ndevu na kutoka hali ya kuwa wamenyoa. Walikuwa wamevaa mavazi ya Kiislamu. Hii leo wamekuwa wanavaa kigeni.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930)
  • Imechapishwa: 30/08/2020