Waislamu wanaoshiriki kwenye bunge hawana mavazi ya Kiislamu.

Msikilizaji: Hawana utu wa Kiislamu.

al-Albaaniy: Wanaonelea ni lazima kuvaa tai ili kuwapaka mafuta. Wao wanafikiria kuwa watawapata watu, lakini wakati huo huo watu ndio huwapata wao.

Msikilizaji: Kuna mmoja katika ndugu zetu alikutana na Tabliyghiy mmoja na kumuuliza la kufanya lau angeliwaona watu wanatukufu kwenye kaburi. Akasema:

“Ningelitufu pamoja nao ili waweze kujisikia. Baada ya hapo ndio ningeliwaeleza kuwa haijuzu, ni shirki na kadhalika.”

Mtu anaweza kulinganisha hili na kuvaa tai kwa ajili ya kuwapaka mafuta?

al-Albaaniy: Ninatarajia hivo, lakini tai ni khatari zaidi. Kwa sababu wanaonelea kuwa hii ni ada, kawaida na ni jepesi na kwamba sisi tunakazia mambo. Huyu Tabliygh anapinga hilo kwa ndani, lakini anafikiria kuwa anawavuta watu kwa kushirikiana nao kwenye upotevu. Hili ni katika ujinga wao. Mola Wetu (´Azza wa Jall) Aliulea Ummah wa Kiislamu kwa kupitia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi Aliposema:

وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا

“Na lau kama Hatukukuthibitisha; kwa yakini ungelikaribia kuelemea kwao kidogo.” (17:74)

Ni matishio makali sana kwa mfano wa watu kama hawa na sio kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanafikiria kuwa watu watavutika nao wakienda kukutana nao namna hii. Ni kinyume chake kabisa. Kuna tofauti kama tulivyosema kati ya hili na kubadilisha staili ya mavazi kwa sababu wanaona kuwa mabadilisho ya staili ya mavazi haina neno yoyote. Ama kuhusiana na kutufu kwenye kaburi, watu hawa wanaonelea kuwa ni dhambi. Kuna tofauti kubwa. Hutomwona karibu yeyote katika al-Ikhwaan al-Muslimuun ambaye ana utambuzi mchache juu ya Sunnah na elimu ya Kiislamu hakuvaa tai na kwenda kinyume na al-Ikhwaan al-Muslimuun wengine wote. Wanaweza kuhesabiwa kwa vidole. Kwa mfano mmoja wao alikuwa ni Shaykh ´Abdullaah ´Azzaam.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930) Tarehe: 1417-04-09/1996-08-24
  • Imechapishwa: 30/08/2020