Wakati bora wa kusoma Suurah “al-Kahf”

Swali: Inasihi kusoma Suurah “al-Kahf” usiku wa kuamkia ijumaa? Je, mtu huyu anapata fadhilah za kusoma Suurah “al-Kahf”?

Jibu: Hapana. Kusoma Suurah “al-Kahf” kunakuwa siku ya ijumaa. Bora ni mtu asome baada ya jua kuchomoza. Una ruhusa ya kusoma kuanzia pale jua linapochomoza mpaka wakati wa kuzama kwa jua. Ukisoma wakati wowote, kuanzia pale wakati wa kuchomoza kwake mpaka wakati wa kuzama kwake, basi imesihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1555
  • Imechapishwa: 25/02/2020