Mtu akihisi dhiki ndani ya swalah basi atambue kuwa huo ni mtihani

Swali: Mimi naswali na namshukuru Allaah kwa hilo. Lakini hata hivyo nahisi dhiki na kutokuwa na raha ndani ya swalah. Naomba maelekezo na Allaah akujaze kheri.

Jibu: Haya ni maradhi miongoni mwa maradhi ya moyo. Mara nyingi sababu yake ni madhambi na upumbaaji. Ambaye kifua chake hakikunjuki ndani ya swalah lililompelekea kuhisi hivo ni upumbaaji, upuuzaji na madhambi yake. Kwa hiyo anachotakiwa ni yeye kutubu kwa Allaah, apambane na nafsi yake, amwombe Allaah tawfiyq na audhuhurishe moyo wake ndani ya swalah. Kwani swalah ni raha na ni tulizo la macho. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tulizo la macho yangu limefanywa ndani ya walah.”

Ni tulizo la macho. Alimwambia Bilaal:

“Tupe raha kwa swalah.”

Swalah ni raha ya mioyo, raha ya dhamira na raha ya macho. Pindi muumini anaingia ndani yake anafurahi, moyo wake unapata utulivu na macho yake yanatulia. Kwa sababu ndio nguzo ya Uislamu. Jengine ni kwa sababu amesimama mbele ya Mola wake. Kwa hiyo anatakiwa kusimama mbele Yake akiwa ni mwenye kunyenyekea. Ndio raha ya moyo, neema ya roho na tulizo la macho. Mtu akihisi dhiki ndani yake basi atambue kuwa huo ni mtihani. Kwa hiyo anachotakiwa ni kujitibu kwa kutubu kwa Allaah, amwombe tawfiyq, amwongoze na amsaidie. Allaah (Jalla wa ´Alaa) anamsamehe yule mwenye kutubia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3709/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D9%84%D8%A7-%D9%8A%D8%AD%D8%B3-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%B7%D9%85%D8%A7%D9%86%D9%8A%D9%86%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%AA%D9%87
  • Imechapishwa: 25/02/2020