Swali: Mwanamke kutoka Uingereza anasema kuwa baba yake amefariki. Amebaki na ami yake lakini mjomba wake ndiye kamuozesha. Je, inajuzu kufanya hivi na ndoa ni sahihi?

Jibu: Hapana. Ndoa si sahihi. Kwa sababu mjomba sio walii wake. Walii zake ni mvulana wake, mvulana wa mvulana wake, baba yake, babu yake upande wa baba, kaka zake, wavulana wa kaka yake au watoto wa ami zake upande wa baba. Aliye karibu zaidi katika wao ndiye atamuoza. Kuhusu wajomba ni ndugu, lakini sio mawalii. Ni lazima ndoa ifungwe upya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017