Usifute kile utachovua


Swali: Nilitawadha kisha nikavaa soksi na viatu. Baada ya hapo nikataka kutawadha upya. Je, nipanguse viatu au nivivue pamoja na kuzingatia ya kwamba pindi ninapoingia msikitini basi huvua viatu hivi na naswali hali ya kuvivua?

Jibu: Hapana, usifute kile utachokivua. Pangusa juu ya kitu imara ambacho hutokivua, nacho ni soksi. Kwa sharti soksi hizo ziwe ni zenye kufunika kile kilicho ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2018