Kitabu hiki – ”Ihyaa´ ´Uluum-id-Diyn” cha Abu Hamiyd al-Ghazaaliy – kimekosolewa kwa panda mbili:

1 – Kuhusiana na kipengele cha kwanza katika kitabu kinachozungumzia ´Aqiydah, anaamini ´Aqiydah ya Ashaa´irah. ´Aqiydah ya Ashaa´irah inatofautiana na ´Aqiydah ya Ahl-ul-Hadiyth na khaswa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah). Anapindisha maana ya Aayah na Hadiyth zinazozungumzia sifa za Allaah (Ta´ala) ikiwa ni pamoja na maneno Yake:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

Anaifasiri Aayah hii kwa tafsiri ya wale waliokuja nyuma.

2 –  Anamili katika Taswawwuf. Alikuwa amezama ndani yake.

[1] 20:05

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (29)
  • Imechapishwa: 06/03/2019