Swali: Inajuzu kwa imamu kuwakatza waombaji msikitini?

Jibu: Akijua kuwa sio wahitaji awakataze. Ama ikiwa hajui kama ni wahitaji au sio wahitaji, asiwakataze. Lakini hata hivyo awakataze kunyanyua sauti na kuwasumbua wenye kuswali. Aimwambie akae chini na watu watampa swadaqah na kwamba hakuna haja ya kuongea na kuhubiri. Baadhi yao wanahubiri na kuwasumbua watu. Wakatazwe haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017