´Umrah ya mwanamke bila ya ridhaa ya mume


Swali: Mwanamke huyu alimuomba mume wake kwenda ´Umrah pamoja naye, akakataa bila ya udhuru. Nikawa nimeenda pamoja na mvulana wangu na nikafanya ´Umrah. Je, ´Umrah yangu ni sahihi na ni mwenye kupata madhambi kwa kutomtii mume wangu?

Jibu: ´Umrah yake ni sahihi lakini anapata madhambi kwa kumuasi mume wake. Kwa kuwa hakumpa idhini. Anapata madhambi kwa hilo. Ama kuhusu ´Umrah ni sahihi pamoja na madhambi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (72) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14085
  • Imechapishwa: 16/11/2014