Umoja ni lazima uwe juu ya haki


Swali: Kupatikana kwa mapote na makundi mbali mbali leo ni katika tofauti ambayo Allaah Amesema juu yake:

كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

“Kila kundi kwa waliyokuwa nayo linafurahia.”? (23:53)

Jibu: Ndio. Tofauti haijuzu kati ya Waislamu. Kukipatikana tofauti katika kuelewana, watu wanatakiwa kurudi katika Qur-aan na Sunnah na wanachuoni na wasuluhishe migogoro hiyo. Ama kuiacha na kusema ´tushirikiane kwa yale tunayoafikiana na tusameheane kwa yale tunayotofautiana`, hili ni batili. Lililo la wajibu ni sisi kurudi kwenye Kitabu cha Allaah:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni (njia) bora na matokeo mazurizaidi.” (04:59)

Mkoseaji anapaswa kurudi kwenye usawa. Hili ndio la wajibu. Kuhusu ushabiki na kusema tusameheane na kila mmoja abaki kwenye mambo yake, hili halijuzu. Ni lazima watu wawe na umoja juu ya haki na kuacha batili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_02.mp3
  • Imechapishwa: 01/07/2018