´Umar bin ´Abdil-´Aziyz au Mu´aawiyah?

Makhaliyfah wane wamesifiwa kuwa ni waongofu kwa kuwa walisimama kwa uongofu (الرشد) ambako maana yake ni kule kuitambua haki na kuifanyia kazi. Wameitwa kuwa ni waongofu kwa kuwa walikuwa wajuzi juu ya haki na wakaitendea kazi. Sifa hii haipewi mwingine isipokuwa hawa wane.

Kuhusiana na ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) kuna tofauti; anahesabika kuwa ni katika Makhaliyfah waongofu au hapana? Wanachuoni wengi ikiwa ni pamoja na Ahmad na wengine wanaonelea kuwa ni katika Makhaliyfah waongofu kwa kuwa ni mtu aliyeitambua haki na kuitendea kazi ilihali upande mwingine watawala wote hawako hivo. Bali miongoni mwao kuko hata ambao asli yao hawatambui haki na kuko ambao wanaitambua haki lakini hata hivyo wanaenda kinyume nayo kutokana na matamanio na sababu nyinginezo.

Hapa kuna tanbihi juu ya masuala ambayo pengine hupitika kwenye ndimi za baadhi ya waandishi maneno ambayo sio ya salama kwa njia ya nafasi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni pale wanaposema kuwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) ni Khaliyfah wa tano. Hili si sawa. Kwa kuwa Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhu) ana manzilah kubwa kuliko ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah). Ingelikuwa kuna ambaye anastahiki kuitwa kuwa ni Khaliyfah wa tano basi angelikuwa ni Mu´aawiyah kwa kuwa yeye ana haki zaidi kwa sifa hii kuliko ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz. Hata hivyo ´Umar [bin ´Abdil-´Aziyz] amesifiwa na kundi katika wanachuoni ya kwamba ni Khaliyfah mwongofu na vilevile Mu´aawiyah kwa kuzingatia ya kwamba watu walikusanyika kwake yeye pia ni Khaliyfah mwongofu. Lakini kwa vile aliacha maamrisho ya ufalme apewe mtoto wake, wanachuoni wakawa wamemzingatia kuwa ni mfalme mwongofu. Yeye (Mu´aawiyah) ndio mfalme bora kabisa wa Waislamu pasina kipingamizi na ni Khaliyfah vilevile kwa kuwa aliwaongoza walio kabla yake juu ya haki. Pamoja na hivyo haitwi kuwa ni Khaliyfah wa tano. Kunaposemwa kuwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) yeye pia ni Khaliyfah mwongofu, hili ni haki. Lakini pamoja na hivyo hakusemwi kuwa ni Khaliyfah wa tano miongoni mwa Makhaliyfah waongofu kwa kuwa Mu´aawiyah ana haki zaidi ya sifa hii lau ingelikuwa inafaa kuitwa hivo. Ama kuhusiana na Makhaliyfah ni wa wanne tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ukhaliyfah wa ki-utume ni kwa miaka thelathini.”

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 396-398
  • Imechapishwa: 13/05/2020