Tunashuhudilia


Dahliyz nilimuuliza Abu ´Abdillaah kama tunawashuhudilia Pepo wale kumi. Akajibu:

“Tunawashuhudilia. Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mnawashuhudilia kwamba wauliwaji wetu kuwa Peponi.”

Ilikuwa idadi kubwa ya watu. Sa´iyd bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nashuhudilia.”

Sa´iyd bin al-Musayyab amesema:

“Ningemshuhudilia mtu yeyote ambaye yuko hai basi ningemshuhudilia Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa).”

Ndipo nikasema:

“Je, akatwe ambaye anashuhudilia?”

Akasema:

“Unakusudia nini?”

Nikasema:

“Nasema yale yaliyosemwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakini hata hivyo nakhitari kutoshuhudilia.”

Akanyamaza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Abiy Harb al-Jarjaara’iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 11
  • Imechapishwa: 19/03/2021