Tufuate jadwali ipi?


Swali: Ufaransa kuna maoni tofauti juu ya nyakati za swalah, khaswa juu ya swalah ya ´Ishaa na Fajr. Tunakaribia mwezi wa Ramadhaan na tunachelea fitina na mpasuko. Je, tufuate jadwali ya chuo cha Fiqh (المجمع الفقهي) au jadwali ya msikiti mkubwa ulioko Paris?

Jibu: Rejeeni katika kituo chenu cha Kiislamu. Rejeeni katika kituo chenu cha Kiislamu. Watatendea kazi jambo la salama zaidi na kufanya lile ambalo ni la lazima.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (63) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16641 Dakika: 1.11.15
  • Imechapishwa: 05/02/2021