Ama masuala ya Televisheni, hii ni propaganda ya maadui wa Uislamu. Hawakutosheka na vyombo vya khabari walivyo navyo; katika radio, swahifa na nyinginezo. Hawakutosheka na haya. Kwani radio kuko watu wanaosikiliza, swahifa kuko watu wanaosoma. Televisheni ni balaa kubwa ilioingizwa katika manyumba ya Waislamu. Sisi hatufuati kichwa mchunga katika Dini ya Allaah na wala hatumuadhimishi kiumbe yeyote kwa hali yoyote haki inapodhihirika kwetu.

Televesheni ina upuuzi na taarabu, picha, mwanaume kumwangalia mwanaume, na mwanamke kumwangalia mwanaume, mafunzo ya kuiba, ufisadi na fikira za kimagharibi. Haya yameingia katika miji ya Waislamu.

Ni wajibu kwa kila Muislamu kutahadharisha Televesheni, kujiweka nayo mbali na aisafishe nyumba yake. Na yule mwenye Imani yenye nguvu na ana uwezo wa kupanda juu ya dari ya nyumba na kuitupa (Televeshini) kwa chini, afanye hivyo. Anatakiwa kuwaiga Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) pindi walipoharamishiwa pombe, waliimwaga ikaenea katika kila njia ya Madiynah mpaka ikaenea kila mahala. Yule atakayemuona mtu au Qaadhiy mwenye kilemba kikubwa kanunua Televesheni na kadanganyika kwa hili masikini mtu huyu na kilemba kikubwa hicho au kadanganyika na ndevu hizo nyingi, kisha sasa ikamdhihirikia kuwa ni Haramu, tunamnasihi kufanya kama tulivyosema. Na mmekwishajua uharamu wake. Apande juu dari ya nyumba yake, kisha aitupe chini. Allaah Awalipe baadhi ya watu wa kheri. Khabari (hii) ilimfikia naye yuko Jeddah.

Kuna mlinganiaji aliyemfikishia naye alikuwa Jeddah na alikuwa na wake wawili. Akawaita wake zake wawili ili wasifikirie kuwa mume wao ni mwendawazimu. Akawaambia: “Mimi ni fulani bini fulani na nina akili zangu, sikilizeni vizuri na msifikirie kuwa nimechanganyikiwa.” Akachukua Televesheni na kuitupa kwa chini, mpaka Allaah Akamstarehesha.

Haijuzu kwetu kuwa na Televesheni ndugu zangu, hata kama ndani yake atajitokeza mtu mwenye ndevu nyingi au mtu mwenye kilemba kikubwa na kutoa Darsa ndani yake. Kinachopaswa kuzingatiwa kuna nini baada ya Darsa (hiyo)? Baada ya Darsa hiyo kuna upuuzi, filamu, sauti ya mwanamke mfitinishaji. Na baada ya Darsa kuna mambo maovu.

Wameleta (wameweka) Darsa hii kwa nini? Wameleta Darsa hii ili kuzichezea akili zangu na zako na ili wazichezee ndevu zangu na zako. Ili tusema: “Lau ingelikuwa ni Haramu asingejitokeza ndani yake Qaadhiy (Shaykh) fulani na Muftiy fulani na mfano wa hayo.”

Dini inachukuliwa kutoka katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haichukuliwi kutoka serikalini wala jamii. Dini haichukuliwi hata ikiwa ni kwa mtu wa Sunnah ambaye umemuona kaiingiza nyumbani kwake, unatakiwa kujua kuwa amekosea. Hatuna nafasi ya kuongelea madhara mengine ya Televesheni.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=163
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 09/11/2014