Tazama ni nani unatangamana na kukaa nae


Hizbiyyuun wanaweza kuwateka baadhi ya wanawake wenye huruma kupitia mikanda inayogawiwa bure. Inazungumzia juu ya mauti, Pepo, Moto… Pasi na kujali itazungumzia nini usijiaminishe. Hatuhitajii mikanda yao. Lau tutakusanya mikanda ya Ahl-us-Sunnah, vitabu, vipeperushi, basi tutapata idadi kubwa kabisa.

´Imraan bin Hittwaan alimuoa binadamu yake ambaye alikuwa ni Khaarijiyyah ili amfanye aweze kuacha Bid´ah yake. Hatimaye mwanamke huyo yeye ndiye akamtoa kwenye Sunnah na kumuingiza katika Bid´ah. Rafiki anaathiri. Tahamaki ghafla ameshakuvuta kwenye Bid´ah bila ya wewe kujua. Methali inayosema kuwa rafiki anaathiri ni hekima na sio Hadiyth. Ni hekima ilio pahala pake stahiki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu anakuwa katika dini ya rafiki yake; hivyo basi mmoja wenu atazame ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake.”

Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy kupitia kwa Abu Hurayrah ikiwa na mlolongo wa wapozi ulio mzuri.

Mtu anakuwa katika dini ya rafiki yake, dini ya kipenzi chake, dini ya anaotangamana nao, dini ya wale anaokaa nao. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… hivyo basi mmoja wenu atazame ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake.”

Ni nani anayekaa naye, ni nani anayetangamana naye na ni nani anayempenda. Tahamaki pasi na kujua ghafla umefungamana naye.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/Dars-14107
  • Imechapishwa: 19/09/2020