Swali: Je, niketi chini au niswali swalah ya mamkuzi ya msikiti katika wakati uliokatazwa baada ya alasiri au alfajiri? Ni ipi dalili kutoka katika Sunnah?

Jibu: Bora ni wewe uswali swalah ya mamkuzi ya msikiti . Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapoingia mmoja wenu msikitini basi asiketi chini mpaka aswali Rak´ah mbili.”

Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa unapaswa kuketi chini kutokana na kughilibu Hadiyth za makatazo kwa sababu ndio sahihi na nyingi zaidi. Pia mwenye kukaa ni sawa na mwenye kuswali ni sawa. Lakini bora ni wewe kuswali Rak´ah mbili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 09/08/2020