Swawm ya Dhul-Hijjah katika masiku ya Tashriyq

Swali: Kuhusu mtu ambaye anafunga masiku meupe afunge tarehe kumi na moja, kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano pamoja na kwamba tarehe kumi na tatu ni katika masiku ya Tashriyq au aifanye swawm yake katika yale masiku kumi?

Jibu: Anauliza kuhusiana na mtu ambaye anafunga masiku meupe, tarehe kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano, kama inafaa katika mwezi wa Dhul-Hijjah kufunga tarehe kumi na tatu? Hapana, haifai. ´Iyd-ul-Adhwhaa inakuwa na masiku matatu. Masiku haya yanaitwa ´masiku ya Tashriyq`. Haijuzu kwa mtu kufunga ndani yake. Isipokuwa yule ambaye anafanya hajj ya Tamattu´ na Qaarin ambaye hakupata kichinjwa, hao inafaa kwao kufunga.

Lakini tunamwambia muulizaji huyu afunge yale masiku kumi ya Dhul-Hijjah; bi maana tarehe moja, mbili, tatu, nne, tano, siku, saba, nane na tarehe tisa. Hayo yatakutosha na kutohitajia kufunga masiku meupe. Mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga kila mwezi masiku matatu. Hazingatii ameyafunga mwanzoni mwa mwezi, katikati yake au mwishoni mwake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1445
  • Imechapishwa: 29/12/2019