Swalah zote kwa wudhuu´ mmoja


128- Nilimuuliza baba yangu kuhusu mtu ambaye anatawadha kwa ajili ya kila swalah. Akajibu:

“Hakuna neno kuswali swalah zote kwa wudhuu´ mmoja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali swalah zote kwa wudhuu´ mmoja siku ya Ufunguzi.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (1/105)
  • Imechapishwa: 24/01/2021