Swalah ya mtu ambaye mara akili inamtoka na mara inamjia

Swali: Mimi ni miongoni mwa watu wanaowatendea wema baba yangu na mama yangu. Nimemsubiria baba yangu na kumshughulikia hospitalini. Kuhusu mama yangu yuko pamoja na mimi nyumbani. Ameshatokwa na akilini; mara zinarudi na mara zinaenda kila wakati. Wakati ninapomwambia mama yangu aswali basi anaswali lakini hata hivyo kwa mfano anaswali Dhuhr zaidi ya Rak´ah nne, mara anazidisha na mara anapunguza. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Allalah (Jalla wa ´Alaa) amesem:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Katika  kile kipindi yuko na akili na anaweza kuzihudhurisha wakati wa swalah, basi unatakiwa kumuamrisha kuswali pindi wakati unapoingia na umsaidie juu ya kuswali. Allaah akujaze kheri na akuwafikishe kwa kuwaangalia na kuwatendea wema. Hichi ni kitendo chema ambacho unalipwa thawabu kwacho. Unatakiwa vilevile kumfunza idadi ya Rak´ah na umzindue juu ya hilo. Kwa msemo mwingine unatakiwa kumsaidia. Aswali kwa kiasi cha uwezo wake. Kwani hakika Allaah haikalifishi nafsi zaidi ya vile inavyoweza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 01/12/2017