Swalah ya kusimama ndani ya chombo cha usafiri

Swali: Kuna mtu anasafiri katika chombo cha usafiri na hawezi kusimama na kuswali. Je, aswali swalah ya faradhi humo katika hali hiyo kabla ya muda kwisha?

Jibu: Kwa nini hawezi kusimama na kuswali? Si yeye ndiye mwenye kumiliki funguo na anaweza kupaki gari na kuswali? Asimame na kuswali. Ama akiwa kwenye boti, kipando, meli au ndege na hawezi kusimama, aswali kwa kiasi na anavyoweza:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Ikiwa yeye ndiye ana maamuzi juu ya kipando, anatakiwa kusimama na kuswali. Ikiwa hana maamuzi yoyote juu yake, aswali vile anavyoweza:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (42) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2011%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/03/2017