Ni lazima kuelekea Qiblah kwa mwenye kuswali ndani ya ndege?

Swali: Ni lazima kwa mtu kuelekea Qiblah akiswali ndani ya ndege?

Jibu: Ndio. Ndani ya ndege kuna nafasi ya kusimama na kuelekea Qiblah; mahali pa kutokea, sehemu ya kupitia katikati ya viti:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Ikiwa hawezi aswali kadri na anavyoweza.

Ikiwa ndege inadema mwishoni mwa wakati wa swalah, aicheleweshe swalah mpaka pale ndege itapodema na aswali pale atapodema. Ikiwa swalah ni katika zile ambazo hazijuzu kuijumuisha na ilio ya baada yake, aswali kadri na hali yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (42) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2011%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/03/2017